MH. HASHIM RUNGWE NA UBWABWA MASHULENI, SERA YA KITAALAMU KWENYE UCHAGUZI 2020
JICHO LA KITAALAMU :
HASHIMU RUNGWE NA SERA YA UBWABWA MASHULENI.
Naandika Magoda Jr .
Kitaalamu sera ya Hashimu Rungwe ya ubwabwa wa moto mashuleni ni moja ya sera bora zaidi kwa mustakabali wa taifa letu na inaendana na hadhi ya taifa la uchumi wa kati wa Tanzania , hakika amefikiria kwa kuweka utaifa mbele kuliko maslahi ya wachache na watanzania wote inabidi tumuunge mkono.
📕 Kitaalamu Hashim Rungwe ametumia lugha ya kisiasa ili kupata umakini wa watu wengi ndio maana katumia neno ubwabwa lakini hoja yake kubwa ni kuhakikisha wanafunzi wetu wanapata chakula bora mashuleni kuanzia chekechea kidato cha sita kwa faida ya mwili na ubongo pia.
📕Duniani kote tafiti zinathibitisha pasi na shaka kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja katika ya chakula bora na ujifunzaji mzuri mashuleni ,lakini pia katika uga wa utatibu wanathibitisha umuhimu wa lishe bora na ukuaji mzuri wa mwili na afya ya akili na hapo ndio Hashim Rungwe amepafikiria zaidi na wengi wameshindwa kumuelewa na akili zikienda kwenye ubwabwa tu.
Kitaalamu hasa katika uga wa elimu hata uwe na walimu laki tano katika shule moja ,uwe na madawati ,vitabu vya kutosha , kama afya ya mwili na akili ya mjifunzaji imezorota basi zoezi la ujifunzaji litakuwa halina mashiko ya muda mrefu kabisa ndio maana Gwiji Hashimu Rungwe kaja na maono ya kitaifa ya chakula bora mashuleni .
📕 Kitaalamu Hashim Rungwe anaungana na mataifa ya uchumi wa kati na wa juu katika utoaji na uhakikishaji wa watoto wanapata chakula bora tena cha moto , na mataifa makubwa kiuchumi yanatambua umuhimu wa lishe bora kwa wanafunzi ndio maana wameweka mkazo hapo Sweden , Marekani , Finland ni baadhi ya mataifa yanayohakikisha wanafunzi wake wanapata lishe bora .
📕 Kitaalamu Hashim Rungwe ametambua kuwa Tanzania hatuna shida ya rasilimali vitu maana Mungu katujalia ila shida ni rasilimali watu makini na bora na kupitia lishe bora taifa litakwenda kupata watu makini sana sababu wengi wa sasa wanakumbwa na udumavu wa mwili na afya ya akili kutokana na athari ya Lishe bora .
📕Hashim Rungwe ameziangalia Kitaalamu shule zetu kama moja ya injini muhimu sana kwa taifa letu ndio maana kaamua aje na sera yenye tija huko na hata mataifa makubwa vetting za viongozi ,maafisa usalama ,wanamichezo huanzia mashuleni na wamewekeza huko kimwili na kiakili pia .
Baba wa taifa la Singapore Lee Kuan Yew aliwahi sema kuwa Shuleni ndio mahali pekee ambapo serikali inauwezo mkubwa wa kuandaa taifa bora kuliko wakiwa nyumbani kwao.
NB: ITOSHE KUSEMA KUWA NINA IMANI NA HASHIM RUNGWE IKIMPENDEZA DKT JPM AMPE NAFASI TULE UBWABWA WA MOTO
Wenu katika kusubiria Dkt JPM akiunga mkono sera ya ubwabwa
Magoda Jr
+255718821168
Mtaalamu
Chiwezi ,Momba.
18/7/2020
Comments
Post a Comment