*PAUL MAKONDA:FANANI ALIYEIMUDU VYEMA HADHIRA YAKE* Naandika Magoda Jr. Moja kati ya sifa bilioni tatu za fanani basi ni kuitambua na kuimudu vyema hadhira yake bila muachano mkubwa , wale ambao walibahatika kuusoma uga wa fasihi wanaweza kuwa mashahidi katika hilo. Pual Makonda au unaweza muita Baba ake na Keegan Kwa nafasi yake aliweza vyema kuendana na mirindimo ya wanadaresalamu na dar es alamu yenyewe na mpaka kijiti kinakabidhiwa kwa mwingine ile hadhi ya jiji la Dar es salaam ilikuwa bado iko juu kileleni. Paul Makonda namuona kama fanani aliyeimudu vyema hadhira yake kwa sababu aliweza fika kujipambanua kulingana na makundi mengi ya wanadaresalamu na alifanikiwa katika hilo maana mkoa wa Dar es salaam sio wa mchezo mchezo . Paul Makonda kijiti chake kimepata mtu mwingine lakini wanadaresalamu na Dar es salaam mchango wake utaendelea kukumbukwa sana na jina lake litabaki mioyoni mwa wanadaresalamu kutoka makundi mbalimbali ya wananchi wa jiji la Dar es...
JICHO LA KITAALAMU : HASHIMU RUNGWE NA SERA YA UBWABWA MASHULENI. Naandika Magoda Jr . Kitaalamu sera ya Hashimu Rungwe ya ubwabwa wa moto mashuleni ni moja ya sera bora zaidi kwa mustakabali wa taifa letu na inaendana na hadhi ya taifa la uchumi wa kati wa Tanzania , hakika amefikiria kwa kuweka utaifa mbele kuliko maslahi ya wachache na watanzania wote inabidi tumuunge mkono. 📕 Kitaalamu Hashim Rungwe ametumia lugha ya kisiasa ili kupata umakini wa watu wengi ndio maana katumia neno ubwabwa lakini hoja yake kubwa ni kuhakikisha wanafunzi wetu wanapata chakula bora mashuleni kuanzia chekechea kidato cha sita kwa faida ya mwili na ubongo pia. 📕Duniani kote tafiti zinathibitisha pasi na shaka kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja katika ya chakula bora na ujifunzaji mzuri mashuleni ,lakini pia katika uga wa utatibu wanathibitisha umuhimu wa lishe bora na ukuaji mzuri wa mwili na afya ya akili n...
Comments
Post a Comment