PAUL MAKONDA: FANANI ALIYEIMUDU VYEMA HADHIRA YAKE
- *PAUL MAKONDA:FANANI ALIYEIMUDU VYEMA HADHIRA YAKE*
Naandika Magoda Jr.
Moja kati ya sifa bilioni tatu za fanani basi ni kuitambua na kuimudu vyema hadhira yake bila muachano mkubwa , wale ambao walibahatika kuusoma uga wa fasihi wanaweza kuwa mashahidi katika hilo.
Pual Makonda au unaweza muita Baba ake na Keegan Kwa nafasi yake aliweza vyema kuendana na mirindimo ya wanadaresalamu na dar es alamu yenyewe na mpaka kijiti kinakabidhiwa kwa mwingine ile hadhi ya jiji la Dar es salaam ilikuwa bado iko juu kileleni.
Paul Makonda namuona kama fanani aliyeimudu vyema hadhira yake kwa sababu aliweza fika kujipambanua kulingana na makundi mengi ya wanadaresalamu na alifanikiwa katika hilo maana mkoa wa Dar es salaam sio wa mchezo mchezo .
Paul Makonda kijiti chake kimepata mtu mwingine lakini wanadaresalamu na Dar es salaam mchango wake utaendelea kukumbukwa sana na jina lake litabaki mioyoni mwa wanadaresalamu kutoka makundi mbalimbali ya wananchi wa jiji la Dar es salaam
Viva Paul Makonda vivaaa. Aluta Continua.
NB: Mkamilifu ni Mungu pekee .
Comments
Post a Comment