JICHO LA KITAALAMU : HASHIMU RUNGWE NA SERA YA UBWABWA MASHULENI. Naandika Magoda Jr . Kitaalamu sera ya Hashimu Rungwe ya ubwabwa wa moto mashuleni ni moja ya sera bora zaidi kwa mustakabali wa taifa letu na inaendana na hadhi ya taifa la uchumi wa kati wa Tanzania , hakika amefikiria kwa kuweka utaifa mbele kuliko maslahi ya wachache na watanzania wote inabidi tumuunge mkono. 📕 Kitaalamu Hashim Rungwe ametumia lugha ya kisiasa ili kupata umakini wa watu wengi ndio maana katumia neno ubwabwa lakini hoja yake kubwa ni kuhakikisha wanafunzi wetu wanapata chakula bora mashuleni kuanzia chekechea kidato cha sita kwa faida ya mwili na ubongo pia. 📕Duniani kote tafiti zinathibitisha pasi na shaka kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja katika ya chakula bora na ujifunzaji mzuri mashuleni ,lakini pia katika uga wa utatibu wanathibitisha umuhimu wa lishe bora na ukuaji mzuri wa mwili na afya ya akili n...
Comments
Post a Comment