JOTO LA UCHAGUZI TANZANIA 2020 MEMBE AJIUNGA ACT WAZALENDO RASMI

.Ni wiki ya HEKAHEKA,
Juma la Kukuru kukara,
Nina maanisha nini?
Twende na Engias Engima aka mtoto wa mwanamke.
Ni kuhusu watia nia ya ubunge kua watia mia.
Ni kwa nini?
Tumeshuhudia watu wengi waliochukuliwa na MAFURIKO 2015,waliorudishwa na UPEPO,si wa kisulisuli
Upepo wa jitahida za serikali safi na nzuri iliojipambanua kufanya vyema 2016-2020.
Wengi wa hawa watia mia,kwamba ni mamia wamegawanyika kwenye makundi yafuatayo:
1:Wakufunzi, professors na PhD,hawa wanahitaji wainuliwe toka mavumbini waketishwe na wafalme,wamechoka kufundisha na kutoa Course  work(ya kuwakata watu alama na kulazimisha wahongwe,hawa ninawahabarisha kwamba wawe tayari kuambulia,kura sifuri hadi tano kama alama za darasani.
2;Watumishi wa uma ambao wamechungulia fursa za teuzi inatokana na wenzao waliowahi kugombea na wakaulamba UDAS,Ukurugenzi,nk miongoni mwa hawa wapo walimu waliochoka na chaki,madaktari waliochoka kututibu,nk
3: Watumishi wa dini mfano wachungaji,maaskofu,mapadre,mashehe,waganga ambao sadaka na michango ya waumini zimekua finyu,nao wanaacha imani wamechungulia mpunga mkubwa wa chombo cha dola.
4:Wastaafu na waliohudumu kwenye utawala na pensheni imekata,hawa wamekumbuka na wanajua walikopata mpunga wametamani tena,nao wapo.
5: Waliopewa madaraka awamu ya tano na wanatamani mpunga mnono zaidi,hawa ni Wakuu wa Mikoa,wakuu wa wilaya na idara mbalimbali.wahenga wa jamii yetu,wanasema punda milia haacha mistari yake,fisi ni fisi tu hata umpe ng'ombe mzima ataacha atakimbilia mfupa.
6.Wakulima,wafugaji,nk hawa nao wamechoka kusikia jembe halimtupi mkulima,nao wapo kwenye kutia mia.
7:Makada watiifu ambao MAFURIKO haijawachukua 2015,wapo waliotia mia(100+) na wapo waliobaki kubung'aa wasipate kujua haya MAFURIKO ya Upepo mzito wa maendeleo ya JPM yametoka.
Orodha ni ndefu,ila liwalo na liwe hofu yangu isije ikawa mtego kwa CHAMA CHA MAPINDUZI,wengine watia mia wasije wakawa wametumwa na mabeberu,halafu wagombea makini wakishapitishwa, MAFURIKO inawachukua tena awamu hii,wakaenda kulalamika kwamba hawajatendewa haki.Tukakosa majimbo.
Mimi ni mawazo yangu finyu,nisipigwe mawe.
Mimi sikutangaza nia,hivyo sipo kwenye waliotia mia(100+
Je jimboni kwako wamefika mia?

Comments

Popular posts from this blog

PAUL MAKONDA: FANANI ALIYEIMUDU VYEMA HADHIRA YAKE

MH. HASHIM RUNGWE NA UBWABWA MASHULENI, SERA YA KITAALAMU KWENYE UCHAGUZI 2020