MHE. STANSLAUS MABULA ATETEA UBUNGE JIMBO LA NYAMAGANA
MHE. STANSLAUS MABULA ATETEA UBUNGE KURA ZA MAONI JIMBO LA NYAMAGANA* Mhe. Stanslaus Mabula aongoza kura za maoni mkutano mkuu wa Jimbo katika mchakato wa awali wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Nyamagana kutafuta mwakilishi atakaye peperusha Bendera Uchaguzi mkuu Octoba 2020. Mhe. Mabula Mbunge anayemaliza muda wake Katika kipindi Cha 2015-2020 amefanikiwa kuongoza Kura za Maoni kwa kupata kura 319, akifuatiwa na John Nzwalile aliyepata kura 54 pamoja na John Nzilanyingi aliyepata Kura 46. Mchakato huo umehusisha wanachama 105 waliojitokeza kwenye kinyang'anilo hicho na kupigiwa kura takribani na wajumbe wa mkutano huo 606. Imetolewa na Ofisi ya Mbunge Jimbo la Nyamagana🇹🇿